Tupo makini na unyanyasaji.
Wanaharakati na watekelezaji wa sheria hutumia Tor kuchunguza unyanyasaji na kuwasaidia waathirika.
Tunafanya nao kazi kuwasaidia kuelewa namna gani Tor inaweza kuwasaidia kwenye kazi zao.
Katika baadhi ya matukio, makosa ya kiteknolojia hutengenezwa na tunawasaidia kusahihishwa.
Kwa sababu baadhi ya watu katika jamii za waathirika hukumbatia unyanyapaa badaka ya huruma, kutafuta msaada kutoka kwa waathirika wenzao inahitaji teknolojia ya kuhifadhi faragha.
Kukataa kwetu kujenga milango ya dharura na udhibiti katika Tor sio sababu ya kutokua na wasiwasi.
Tunakataa kudhohofisha Tor kwa sababu itadhuru jitihada za kuzuia unyanyasaji wa watoto na biashara haramu ya binadamu katika dunia, huku ikiondoa nafasi salama ya waathirika mtandaoni.
Wakati huo, wahalifu bado wanaweza kupata vifaa vya mtandao, kuiba simu, kudukua akaunti zinazoendeshwa, mfumo wa posta, wasafirishaji, wala rushwa na teknolojia yeyote ambayo imejitokeza katika maudhui ya biashara.
Kuna watu waliojihusisha mapema na teknolojia.
Katika kuliangazia hili, ni hatari kwa watunga sera kudhani kuwa kudhibiti na kuficha kunatosha.
Tunavutiwa zaidi na juduhi za kuwasaidia kusimamisha na kuzuia unyanyasaji wa watoto kuliko kuwasaidia wanasiasa kupata alama kwa wapiga kura kwa kuificha.
Nafasi ya rushwa ni maalum katika usumbufu: Tazama ripoti hii ya Umoja wa Mataifa Nafasi ya Rushwa katika Usafirishaji haramu wa Binadamu.
Mwisho, ni muhimu kuzingatia dunia ambayo watoto watahesabika kama watu wazima wanapokiuka sera kwa kutumia majina yao.
Watatushukuru kama hawawezi kutoa maoni yao salama kama watu wazima?
Vipi kama wanajaribu kufichua kushindwa kwa serikali kuwalinda watoto wengine?