Ikiwa upatikaji wako wa mtandao haujadhibitiwa, unapaswa kuzingatia kusanikisha na kuboresha Snowflake ili kuwasaidia watumiaji katika udhibiti wa mtandao. Unapoendesha Snowflake kwenye kivinjari chako cha kawaida, utakuwa na proksi ya trafiki kati ya watumiaji waliodhibitiwa na nodi ya kuingia kwenye mtandao wa Tor na hiyo ndiyo yote.

Kwa sababu ya udhibiti wa seva za VPN katika baadhi ya nchi tunakuomba usiendeshe proksi ya snowflake wakati umeunganishwa kwenye VPN.

Ongeza-katika

Kwanza hakikisha unawezesha WebRTC. Halafu unaweza kusanikisha hii uenezi wa Firefox au uenezi wa Chrome ambayo itakufanya wewe kuwa Snowflake proxy. Pia inaweza kukutaarifu kuhusu watu wangapi uliwasaidi katika masaa 24 yaliyopita.

Kurasa ya tovuti

Katika browser ambapo WebRTC imewezeshwa: Kama hutaki kuongeza Snowflake katika browser yako, unaweza kuingia katika https://snowflake.torproject.org/embed na ugeuze kitufe ili kuchagua kuingia kuwa proxy. Huwezi kufunga kurasa kama unataka kubakiza Snowflake proxy.