Wasiliana

Kwa muda mrefu, jumuiya ya Tor imekuwa ikiendesha shughuli nyingi siku hadi siku kwa kutumia mtandao wa IRC unaojulikana kama OFTC. IRC imefanya kazi vizuri na sisi, na jamii yetu katika IRC imekuwa ikibadilika kadri miaka inavyosonga mbele na watu wapya kujiunga na njia mpya kuibuka kwa mahitaji maalum ndani ya shirika.

Bridge yenye namba nne

Jumuiya ya Tor inafungua mazungumzo yake ya kila siku kwa kuunganisha jumuiya yetu ya IRC kwenye mtandao wa Matrix. Kwa watumiaji wa kawaida wa Tor, inamaanisha unaweza wasiliana na sisi kwa kutumia programu tumizi rafiki kama Element. #tor:matrix.org au kituo cha #tor IRC vimeunganishwa: popote utakapochagua kutumia, ujumbe wako utasambazwa kwenye jukwaa zote.

Kujiunga na mazungumzo ya wachangiaji wa Tor katika Matrix, unahitaji kuwa na akaunti ya Matrix, watoa huduma kadhaa wanaweza kukupatia. Mojawapo ya haya ni Matrix.org Foundation, ambayo inaruhusu watu kusajili akaunti bure. Unaweza kusajili akaunti katika app.element.io.

Mara tu ukiwa na akaunti ya Matrix, unaweza jiunga Tor Matrix space ili uperuzi Tor rooms, au ujiunge moja kwa moja katika room #tor:matrix.org user support.

Mtandao wa OFTC IRC

Mbadala, ikiwa unataka kutumia IRC unaweza OFTC's web IRC client:

  1. Fungua OFTC webchat

  2. Jaza nafasi zilizowazi:

    NICKNAME: Chochote unachohitaji, lakini chagua nickname (nick) sawa kila muda tumia IRC kuongea na watu kwenye Tor. Ikiwa nick yake imeshatumiwa, utapokea ujumbe kutoka katika mfumo na unapaswa kuchagua nick nyingine.

    CHANNEL: #tor

  3. Bonyeza kuingia

Hongersa! Sasa upo katika IRC.

Baada ya sekunde chache, utaingiza #tor kiotomatiki, ambayo ni chumba cha mazungumzo cha watengenezaji wa Tor, waendesha relay na wanajumuiya wengine.pia kuna watu aina mbalimbali ya watu katika Tor.

Unaweza kuuliza swali katika sehemu ya kuandikia chini kioo cha mbele, Tafadhari usiombe kuuliza, uliza tu swali lako.

Watu wanaweza kujibu mara moja, au kunaweza tokea ucheleweshaji (baadhi ya watu wamejiorodheshwa katika njia za usambazaji lakini wapo mbali na keyboards zao na wanarekodi shughuli za njia za usambazaji ili kuzisoma baadae).

kama unataka kuwasiliana na mtu maalum, anza maoni yako na jina lao na watapokea taarifa kuwa mtu fulani anajaribu kuwasiliana nao.

OFTC mara nyingi hairuhusu watu kutumia webchat zao na Tor. Kwa sababu hii, na kwa kuwa watu wengi huishia kuipendelea yenyewe hata hivyo, unapaswa pia kuzingatia kutumia IRC client.

Channel ya #tor-project ni sehemu ambapo watu wa Tor hufanya mazungumzo na huratibu kazi za Tor za kila siku. Ina wanachama wachache zaidi ya #tor na imejikita zaidi katika kutenda kwa mikono. Unakaribishwa kujuiunga na channel hii. Ili kupata #tor-project, nickname yako inapaswa kusajiliwa na kuthibitishwa.

Hapa ni jinsi ya kufikia #tor-project na njia zingine za usafirishwaji zilizosajiliwa.

Sajili nickname yako

  1. ingia kwa #tor. angalia ni jinsi gani ntawasiliana na Tor Project teams?

  2. Halafu, bonyeza kwenye neno "Status" upande wa juu kushote kwenye kioo cha mbele.

  3. kwenye kompyuta yako bonyeza chini ya ukurasa, andika **/msg nickserv SAJILI jina lako na neno siri la anwani yako

  4. Gonga enter.

kama zote zikienda vizuri, utapokea ujumbe kuwa umesajiliwa.

Mfumo unaweza kusajili nick_ yako badala ya nick yako.

Ikiwa ndivyo, endelea na hivyo lakini kumbuka wewe ni mtumiaji_ na si mtumiaji.

Kila muda unapoingia katika IRC, kutambua usajili wako wa jina bandia, andika:

/nick yournick

/msg nickserv IDENTIFY YourPassWord

Ninawezaje kuthibitisha nickname yako

Baada ya kusajili nickname yako, ili kupatikana katika #tor-project na njia zingine za usafirishwaji zinazolindwa, nickname yako lazima iwe verified.

  1. Nenda kwenye https://services.oftc.net/ na fuata hatua katika sehemu ya 'kuhakiki akaunti yako'

Rudi kwenye ukurasa wa wavuti wa IRC ambapo umesajiliwa na uandike:

/msg nickserv checkverify

  1. Bofya ENTER.

  2. Ikiwa yote yapo sawa, utapokwa ujumbe unaosema:

*!NickServ*checkverify

Usermodechange: +R

!NickServ- Successfully set +R on your nick.

Jina lako bandia limethibitishwa!

Sasa, kujiunga na #tor-project, unapaswa kuandika:

/join #tor-project na gonga enter.

Utaruhusiwa kuwa katika channel. ikiwa umeambia, Hongera!

Hata hivyo, ikiwa unakwama, unaweza kuomba msaada katika #tor channel.

Unaweza kubadilisha kati ya vituo kwa kubonyeza majina tofauti ya kituo kwenye upande wa kushoto juu ya window ya IRC.

Tor inategemea msaada wa watumiaji na wajitoleaji ulimwenguni kote kutusaidia kuboresha programu yetu na rasilimali, kwa hivyo maoni yako ni muhimu sana kwetu (na kwa watumiaji wote wa Tor).

fomu ya mrejesho

wakati Unatutumia maoni au kutoa taarifa kuhusu hitilafu, tafadhali jumuisha na vingine iwezekanavyo:

  • mfumo wa uendeshaji unaotumia
  • Toleo la Tor Browser
  • Kiwango cha ulinzi wa Tor Browser
  • Hatua kwa hatua jinsi ya kupata suala hilo, ili unaweza kulizalisha tena (kwa mfano Nimefungua kivinjari, nikaandika url, nikabofya (i) icon, kisha kivinjari changu kikapotea)
  • skrini yenye tatizo
  • kumbukumbu

namna ya kutufikia

Kuna njia mbalimbali za kuwasiliana nasi,tafadhali chagua ipi itakufaa zaidi.

jukwaa la Tor

Tunashauri kuomba msaada katika Jukwaa laTor. Utahitaji kutengeneza akaunti ili kuwasilisha mada mpya. Kabla hujauliza, tafadhari hakiki miongozo yetu ya majadiliano. Kwasasa, kwa majibu ya mwisho, tafadhali andika kwa kingereza. Ikiwa umepata programu iliyoharibika, tafadhari tumia GitLab.

#### Gitlab

Kwanza, angalia kama tatizo limejulikana. Unaweza kutafuta na kusoma matatizo katika https://gitlab.torproject.org/. Kuunda jambo jipya, tafadhaliomba akaunti mpya kuipata Tor Project's GitLab haraka na tafuta hifadhi sahihi kutoa taarifa ya tatizo. Tunafuatilia matatizo yote yahusianayo na Tor Browser Tor Browser issue tracker. Matatizo yahusianayo na tovuti yetu yanatakiwa kujazwa katika Kinasa matatizo ya tovuti.

Telegram

Ikiwa unahitaji kusanikisha au troubleshooting Tor Browser na Tor Forum ikizuiliwa au kudhibitiwa mahali ilipo, unaweza kutufikia katika Telegram https://t.me/TorProjectSupportBot. Mtaalam wa msaada wa Tor atakusaidia.

whatsApp

Unaweza kuwasiliana na nasi kwa kutuma ujumbe wa maandishi katika namba yetu ya WhatsApp: +447421000612. Huduma hii inapatikana tu kwa ujumbe wa mandishi; video au simu hazijawezeshwa.

signal

Unaweza kupata msaada kwa kutuma ujumbe wa maandishi katika namba yetu ya Signal: +17787431312. Signalni programu ya matumizi ya bure na imelenga ufaaragha kwa watumiaji. Huduma hii inapatikana tu kwa ujumbe wa mandishi; video au simu hazijawezeshwa. Baada ya kutuma ujumbe,watu wetu wa msaada watakusaidia kutatua tatizo.

barua pepe

Tutumie barua pepe kwa frontdesk@torproject.org.

Katika kichwa cha habari cha barua pepe yako, tafadhali tujulishe unatoa taarifa ya kitu gani. Namna ambavyo kichwa cha habari cha barua pepe kinakuwa mahususi mfano. "Kushindwa kuunganishwa", "mrejesho katika tovuti", "Mrejesho katika Tor Browser, "Nahitaji bridge"), ndivyo itakavyokuwa rahisi kwetu kuelewa na kufuatilia. Wakati mwingine tunapopokea barua pepe zisizo na kichwa cha habari,huingia katika barua pepe zisizothibitishwa na tunashindwa kuziona.

Kwa majibu ya haraka, tafadhari andika kwa Kiingereza, Kihispania, na/au Kireno ikiwa unaweza. Kama hakuna lugha unayoielewa kati ya hizi, tafadhali andika kwa lugha yoyote unayoweza, lakini jua kwamba muda kidogo kujibu sababu tutahitaji msaada wa kutafsiriwa ili kuelewa.

blog ya kuweka maoni

Unaweza kuacha maoni kwenye chapisho la blogu linalohusiana na suala au mrejesho unayotaka kutolea taarifa. Ikiwa hakuna chapisho katika suala lako, tafadhari wasiliana nasi kwa njia ingine.

IRC

Unaweza kutupata kupitia #tor kwenye OFTC ili kutupatia maoni au kuripoti makosa. Hatujibu mara moja, lakini tunachunguza orodha ya kazi zilizobaki na tutakujibu kadri tunavyoweza.

Jifunze jinsi ya kujiunga katika OFTC servers.

orodha ya barua pepe

Kwa kutoa ripoti masuala au majibu ya kutumia orodha ya barua pepe, tunapendekeza kwamba ufanye hivyo kwa ile inayohusiana na kile ambacho ungependa kuripoti. Saraka iliyokamilika katika orodha yetu ya barua pepe inaweza kupatikana hapa.

Kwa majibu au masuala yanayohusiana na tovuti yetu: ux

Kwa mrejesho na masuala yahusuyo kutumia Tor relay: tor-relays

toa taarifa ya kiusalama

Ikiwa umepata suala la kiusalama, tafadhari tutumie barua pepe security@torproject.org.

Ikiwa unataka kusimba barua pepe yako, unaweza kupata funguo la umma ya OpenPGP kwa anwani hii kutoka keys.openpgp.org. Here is the current fingerprint:

  pub   rsa3072/0x3EF9EF996604DE41 2022-11-15 [SC] [expires: 2024-12-11]
      Key fingerprint = 835B 4E04 F6F7 4211 04C4  751A 3EF9 EF99 6604 DE41
  uid Tor Security Contact <security@torproject.org>
  sub   rsa3072/0xF59EF1669B798C36 2022-11-15 [E] [expires: 2024-12-11]
      Key fingerprint = A16B 0707 8A47 E0E1 E5B2  8879 F59E F166 9B79 8C36

Ikiwa unapenda kushiriki katika programu yetu ya bug bounty, tafadhari kuwa makini, kuwasilisha suala la usalama katika tovuti ya watu wengine hubeba hatari fulani ambayo hatuwezi kuidhibiti, ndio matokeo tunapendelea kuripoti moja kwa moja.