Wakati mwingine, baada ya kutumia Gmail kwenye Tor, Google inawasilisha tarifa kwamba huenda akaunti yako imeingiliwa.
Sehemu ya taarifa huorodhesha mfululizo wa anwani za IP na maeneo ulimwenguni sasa hutumika kupata akaunti yako.
Kwa ujumla, hii ni kengele isiyosahihi: Google iliona kundi lililoingia katika sehemu tofauti, kama matokeo ya kuendesha huduma kupitia Tor, na kuamua ilikua wazo zuri la kuhakikisha akaunti itafikiwa na mmiliki wake halali.
Japokuwa hii inaweza kuwa ni kutokana na utumiaji wa huduma kupitia Tor, hii haimaanishi unaweza kudharau angalizo.
Inawezekana ni uwongo chanya, lakini haiwezi kwa kuwa inawezekana kuna mtu ameteka cookie zako za Google.
Utekaji wa cookie unawezekana kwa njia ya kuipata compyuta yako au kuangalia upekuzi wa mtandao wako.
Kwa nadharia,ufikiaji wa kawaida pekee unaweza kuelewana na mfumo wako kwasababu Gmail na huduma za kipekee zinzweza kukutumia cookie juu ya muunganiko wa SSL.
Kwa vitendo, alas, ni way more complex than that.
Na kama kuna mtu ameiba cookie zako za Google, wataishia kuingia kwenye sehemu zisizo za kawaida (pia wanaweza wasiingie). Kwa ufupi ni kwamba ukiwa unatumia Tor Browser, mbinu hii ya ulinzi ambayo Google hutumia haikufai, kwa sababu imejaa chanya za uwongo. Unatakiwa utumie mbinu nyingine, kama vile kuona kama kuna kitu chochote kinaonekana cha ajabu katika akaunti, au kinaonekana katika hifadhi ya waliongia hivi karibuni na unashangaa kama umeingia katika muda huo.
Hivi karibuni, watumiaji wa Gmail wanaweza kuwasha hatua ya 2 ya uthibitishho katika akaunti zao kuongeza safu ya ziada ya ulinzi.