Tor Metrics

Kwa kweli, hatuhesabu watumiaji, lakini tunahesabu maombi kwenye saraka amabyo mtumiaji husasisha mara kwa mara orodha yake ya relay na kukadiria namba ya watumiaji isiyo ya moja kwa moja kutoka hapo.

Hapana, lakini tunaweza kuona sehemu gani ya folda zilizoripoti, na kisha tunaweza kutathmini jumla ya idadi kwenye mtandao.

Tunaweka katika dhana ya kuwa wastani wa watumiaji hufanya maombi 10 kila siku. Mtumiaji wa tor aliunganishwa masaa 24 hufanya maombi 15 kwa siku, lakini sio watumiaji wote waliounganishwa masaa 24, hivyo tunachagua wastani wa watumiaji 10. Tunagawanya maombi ya saraka na kuzingatia majibu kama namba ya watumiaji. Njia nyingine ya kuiangalia, ni kwamba tunadhania kuwa kila ombi huwakilisha mtumiaji ambaye yupo mtandaoni kwa masaa kumi ndani ya siku moja, kwa hivyo ni masaa 2 na dakika 24.

Wastani wa idadi ya watumiaji wanaotumia huduma kwa wakati mmoja, iliyokadiriwa kutokana na data zilizokusanywa kwa siku moja. Hatuwezi kusema ni watumiaji wangapi tofauti wapo.

Hapana, Relay ambayo inaripoti maombi ya takwimu hizi kwa ujumla katika nchi husika katika kipindi cha masaa 24. Takwimu tutazozihitaji kukusanya kwa namba za watumiaji katika lisaa itakuwa na maelezo mengi na kuwaweka watumiaji katika hatari.

Halafu tunahesabu hawa watumiaji kuwa kitu kimoja, Ni kweli tunahesabu watumiaji, lakini ni angavu zaidi kwa watu wengi kufikiria watumiaji, ndio maana tunasema watumiaji na sio wateja.

Hapana, kwa sababu mtumiaji huyo huwa anasasisha orodha ya relays ya mawasiliano mara nyingi kama mtumiaji ambaye habadilishi anwani yake ya IP kwa siku.

Viongozi hupatia ufumbuzi anwani za IP kuwa nambari za nchi na kuziripoti kwa muundo wa kikundi. Hii ni moja ya sababu kwa nini tor inakuja na kifurushi cha data ya GeoIP.

bridges chache sana yanaripoti data juu ya usafirishaji au toleo la IP hadi sasa, na kwa chaguo-msingi tunazingatia maombi ya kutumia itifaki ya OR ya chaguo-msingi na IPv4. Marudio ya ripoti za bridges haya yatakapowasilishwa tena, idadi hizo zitakuwa sahihi zaidi.

Relay na bridges hutoa ripoti ya baadhi ya data katika vipindi vya masaa 24 ambavyo zinaweza kuisha muda wowote.
Na baada ya muda kama huo kukamilika relay na bridge yanaweza kuchukua masaa 18 mengine kutoa ripoti ya data.
Tulitenga siku mbili zilizopita kutoka kwenye graph, kwa sababu tunahitaji kuepuka sehemu ya data iliyopita katika graphu inayoonesha mabadiliko ya sasa ambayo ni kwa kweli ni mabaki ya algorithm.

Sababu ni hii tunachapisha namba za watumiaji pale tu tunapokuwa na ujasiri wa kutosha kuwa hawawezi badilika tena. Lakini kwa kawaida inawezeka saraka hiyo inaripoti data kwa muda mfupi baada ya kuwa na ujasiri wa kutosha, lakini ambayo ilibadilisha graphu kidogo.

Tunayo nyaraka za maelezo kutoka kabla ya wakati huo, lakini nyaraka hizo hazikujumuisha data yote tunayotumia kupima idadi ya watumiaji. Tafadhali tafuta tarball ifuatayo kwa maelezo zaidi:

tarball

Kwa watumiaji wa moja kwa moja, tunajumuisha saraka zote ambazo hatukuzifanyia kazi katika mbinu ya zamani. Pia tunatumia historia ambayo imekusanya bytes zilizoandikwa na kujibu maombi ya saraka, ambayo ni sahihi zaidi kuliko kutumia historia ya kawaida ya byte.

oh, hio ni utofauti wa historia nzima tumeandika ukurasa mrefu wa 13tchnical report inayoelezea sababu ya kuacha kutumia njia ya awali.
Kwa ufupi: Katika njia ya zamani tulipima kitu kisicho sahihi, na sasa tunapima kitu sahihi.

Tunatumia mfumo wa kugundua udhibiti unaotegemea kutofautiana ambao unachunguza idadi ya watumiaji iliyokadiriwa kwa siku kadhaa na kutabiri idadi ya watumiaji katika siku zijazo. Ikiwa idadi halisi iko juu au chini, hii inaweza kuashiria tukio la ufinyu wa uhuru wa kujieleza au kuachiliwa kwa udhibiti. kwa maelezo zaidi, angalia technical report.